GAMBO NA KAWAIDA WAONGOZA PARADE YA MAMIA YA ‘BODABODA’ KUELEKEA MKUTANO WAO WA MWAKA

0

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akiambatana na Comrade Mohammed Kawaida, Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania wakiwaongoza Mamia ya Vijana wa Mkoa wa Arusha wanaojishughulisha na Biashara ya usafirishaji abiria kupitia Pikipiki (Bodaboda) kuelekea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Jijini Arusha AICC kwaajili ya Kuhudhuria Mkutano Mkuu maalum wa Elimu ya Ushirika, elimu ya mikopo pamoja na uzinduzi wa Mfumo wa kidigitali katika utambuzi na uendeshaji wa Biashara ya usafirishaji. Mgeni rasmi kwenye Mkutano huo ni Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mohammed Kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *