DKT. ASHATU ATANGAZA NEEMA KWA WAFUGAJI, ATOA SALAMU ZA RAIS SAMIA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo tarehe 20 Disemba, 2024 ametembelea kikundi cha ufugaji samaki kwa njia ya cha Mama Samia ambao ni wanufaika wa Mradi wa Vizimba katika Mkoa wa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Ashatu amezindua zoezi la uuzaji wa samaki ambazo zimeanza kuvunwa katika Vizimba hivyo.
Katika salamu zake, Dkt. Ashatu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ambapo amewataka Watanzania kuendelea kuinga mkono Serikali katika jitihada zake za kuwakwamua kiuchumi wananchi.