NHC YAPEWA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA WA NYUMBA BORA ZA MAKAZI

0

Shirika la Nyumba la Taifa – NHC limepewa tuzo ya mshindi wa kwanza wa nyumba bora za makazi kwa mwaka 2024 na East Africa Building and Construction Awards 2024.

Meneja Habari na Uhusiano – NHC Bw. Muungano Saguya amepokea tuzo hiyo kutoka kwa Bi. Faith Selema wa kampuni ya Corporate Solution Worldwide – CSW ambao walikuwa moja ya waandaji wa tukio la utoaji wa tuzo hizo.

Tuzo hiyo inalenga kutambua na kuhamasisha ubora, ubunifu wa sekta ya ujenzi katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na miundombinu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *