MOROGORO DC WATAKIWA KUANDIKA ANDIKO UJENZI WA STENDI

0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemwelekeza mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero mkoa wa Morogoro kuandika andiko maalum la mradi wa ujenzi wa standi ya mabasi Manyinga ili kuondoa adha ya miundombinu wanayokutana nayo wananchi katika kipindi cha mvua.

Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea stendi hiyo na kukuta hali isiyoridhisha huku Halmashauri ikiendelea kutoza mapato katika standi hiyo.

“Mkiacha utaratibu ambao huwa mnaufanya wa kutenga mapato ya ndani ambayo mnatenga bajeti kwaajili ya kufanya maendelezo madogo madogo kuna utaratibu mwingine mnaweza kuutumia ambao ni kuandika andiko la mradi kwasababu stendi hii inaonekana inaweza kuwa mradi wa kuzalisha mapato mengi zaidi kwaajili ya Halmashauri kwasababu ya shughuli nyingi za kiuchumi zinazofanyika” amesema

Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amewaahidi wananchi wa Mvomero kuwa serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Manyinga-Madizini yenye urefu wa kilomita 3.9 ambapo serikali itatenga fedha taktibani bilioni sita kawajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

Kwaupande wake mbunge wa Jimbo la Mvomero Mhe. Jonas Van Zeeland ameiomba serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni hitaji la muhimu la kiuchumi kwa wakazi wa Mvomero.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *