BILIONEA MULOKOZI ASHUSHA HELICOPTER NA PORCHE MPYA
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd David Mulokozi ameiongeza Helicopter 🚁 na gari aina ya Porche katika list ya vyombo binafsi vya usafiri ambavyo anavitumia katika shughuli mbalimbali.
Hili linakuwa tukio lingine kubwa la kimafanikio kwa Mr David Mulokozi linaloufunga mwaka huu wa 2024 baada ya kuitikisa mitandao ya kijamii alipoutambulisha mjengo wake wa kifahari mapema january mwaka huu.
Baada ya kutua na chopa yake hiyo katika uwanja wa Tanzanite kwaraa Manyara, Mulokozi ameeleza kuwa upo uhitaji wa uwanja wa ndege katika mkoa wa Manyara ambapo pia amesema kuwa helicopter 🚁 hiyo itamsaidia kurahisisha shughuli zake za kibiashara.