DKT. TULIA AWATEMBELEA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA UYOLE YA KATI

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini,  Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 13 Disemba, 2024 amewatembelea Wafanyabiashara wa Soko la Uyole ya kati, Kata ya Iganjo Jijini Mbeya ili kujionea mazingira ya kazi ya Wafanyabiashara hao.

Pamoja na mambo mengine,  Wafanyabiashara hao wamempongeza na kumshukuru Dkt.Tulia kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo la Mbeya Mjini ikiwa ni pamoja na hatua alizozichukua za kuwakarabatia soko lao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *