MHE. MAHUNDI ACHANGIA KIKUNDI CHA GWALUGANO ISANGE MIL. 3.4 NA TOFALI 1000

0

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameunga mkono juhudi za Kikundi cha UWT Gwalugano Isange chenye mtaji wa shilingi milioni tisini huku akikichangia shilingi milioni tatu na laki nne pia tofali elfu moja za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mradi.

Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wanawake kupendana na kuwataka waendelee kuwahamasisha wengine kujiunga ili kila mwanamke amiliki uchumi wake ambapo amewataka wanawake kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri.

Mbali ya kukipongeza kikundi hicho amesema changamoto wazichukulie kama fursa akikazia kampeni yake ya wanawake na uchumi pia akiwahimiza kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Sanjari na hilo amempongeza Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunga mkono wanawake hao kwa kuwachangia shilingi 3m.

Taarifa ya kikundi cha Gwalugano Isange imesomwa na Katibu Anna Katobe ikionesha mafanikio ya kukusanya jumla ya shilingi milioni tisini huku ikikabiliwa na upungufu wa mtaji.

Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Mwakibete amempongeza Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa unyenyekevu mkubwa na moyo wake wa kuwainua wanawake.

Neno la shukrani limetolewa na Rhoda Tusajigwe kwa niaba ya kikundi kwani kupitia mchango wake kikundi kitazidi kupiga hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *