WAZIRI WA AFYA AWATEMBELEA MAJERUHI WA AJARI BASI LILOKUWA LIMEBEBA WABUNGE

0

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama awajulia hali wagonjwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa wakiwemo wabunge 22 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wamepata ajali katika eneo la Mbande, Kongwa Mkoani Dodoma baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na Lori.

Waziri Mhagama amefika katika hospitali hiyo leo Disemba 06, 2024 kwa lengo la kuwaona wagonjwa waliolazwa wakiwemo wabunge.

“Hospitali ya Benjamini Mkapa imepoekea majeruhi 22, wakiume Tisa na wanawake 13, tumamshukuru Mungu wote wapo hai na wanaendelea vizuri kwa kupata huduma ikiwemo huduma za uchunguzi,” amesema Waziri Mhagama

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mhagama ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari kuendelea kuwasimamia kwa kuwapatia matibabu vizuri wagonjwa wote waliopo katika hospitali hiyo.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Afya ikiwemo hospitali hii ambapo tuna mashine za uchunguzi za kutosha, maabara ambazo zimekua msaada mkubwa sana kwa watanzania wote wanaokuja kupata matibabu katika hospitali hii,” amesema Waziri Mhagama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *