TCAA YAWAFIKIA ZAIDI YA WANAFUNZI 300 ZIARA SHULE ZA SEKONDARI DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imewafikia zaidi ya wanafunzi 300 wa shule za sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaam katika ziara yake ya shule mbalimbali walizozitembelea kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala ya usafiri wa anga.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mwandamizi Elimu na Uchechemuzi kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga, Bi. Debora Mligo katika wiki ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Anga Duniani itakayoadhimishwa Desemba 7 mwaka huu, alipotembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Kwembe iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hizo zilizoanza mapema wiki hii, shule za Sekondari za Kibasila, Jangwani, Makongo na Kwembe zimefikiwa.