MRADI WA SAMIA HOUSING SCHEME, UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 74

0

Mradi wa Samia Housing Scheme, ulioko Kawe jijini Dar es Salaam, unaendelea kwa kasi kubwa huku ujenzi ukiwa umefikia asilimia 74. Hali ya sasa inaonyesha kazi za hatua za mwisho (finishing) zinaendelea kwa umahiri wa hali ya juu.

Kwa sasa, mafundi wanakamilisha uwekaji wa madirisha, milango, makabati, na tiles katika majengo yanayojengwa, kuhakikisha kuwa yanakidhi viwango bora vya ubora na uimara. Huu ni mradi wa kihistoria unaolenga kujenga nyumba 5,000 kwa awamu, ukiwa na bajeti ya takriban shilingi bilioni 466 (sawa na dola za Kimarekani milioni 200).

Mradi huu ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya nyumba nchini, ukiongozwa na dhamira ya kuboresha makazi kwa Watanzania. Mbali na hatua zinazoendelea Kawe, maandalizi ya miradi mingine yanaendelea kwa kasi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba 100 jijini Dodoma, nyumba 560 eneo la Kawe, na nyumba 400 katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Lengo la miradi hii ni kutoa suluhisho la makazi bora, yenye gharama nafuu, na yanayofaa kwa mahitaji ya jamii, sambamba na kukuza uchumi wa nchi kupitia ajira na sekta za huduma zinazohusiana na ujenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *