KIKAO CHA KAMISHENI MPYA YA TUME YA MADINI CHAFANYIKA

0

Leo Desemba 05, 2024 kimefanyika kikao cha kwanza cha Kamisheni ya Tume ya Madini tangu kuteuliwa kwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Madini, Janet Reuben Lekashingo kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hicho pia kimeshirikisha Makamishna wa Tume na Menejimenti kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo mwaka.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wake, Janet Lekashingo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini hasa kwenye eneo la ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini, kuimarika kwa usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na mchango wa kampuni za madini kwa Jamii.

Kupitia kikao hicho mikakati mbalimbali imewekwa kupitia Kamati za Ufundi, Rasilimaliwatu, Fedha na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *