NAFASI ZA KUPANGA JENGO LA MUTUKULA COMMERCIAL COMPLEX BADO ZIPO

0

Nafasi za kupanga kwenye jengo la biashara la Mutukula Commercial Complex lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa – NHC mita chache kutoka mpaka wa Tanzania na Uganda bado zipo, yanakaribishwa makampuni, taasisi za fedha, wajasiriamali, maduka ya nguo, maduka ya dawa, kampuni za simu nk kwa ajili ya kupanga katika jengo hilo kubwa lenye ghorofa mbili na miundombinu rahisi kwa watumiaji na wateja.

Baadhi ya wafanyabishara wameshaanza kutoa huduma huku wananchi wakiipongeza NHC kwa kuweka kitega uchumi hicho ambacho kinakidhi upatikanaji wa mahitaji mbalimbali sehemu moja.

Katika kuhakikisha wananchi wananufaika na jengo hilo, NHC imetoa punguzo la kodi fika ofisi za NHC Mkoa wa Kagera au ofisi zozote za Shirika la Nyumba la Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *