TOTALENERGIES YASAIDIA KUIMARISHA ELIMU YA MTOTO WA KIKE

0

Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd kwa kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo tarehe 22 Novemba 2024 imekabidhi katoni 360 za taulo za kike zenye thamani ya Sh. Milioni 25.5 kwa shule 4 za sekondari.

Shule za sekondari zilizonufaika na msaada huo wa taulo za kike ni ; Lemura ya Hai, Kilimanjaro, Sitalike ya mkoani Katavi, Manunus Mkomboss ya Same, Kilimanjaro na Isack Kamwelwe ya mkoani Katavi. Zaidi ya wanafunzi 1,200 watanufaika kwa mwaka mzima.

Mwaka huu kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd kupitia Mfuko wa Elimu waTaifa imetoa jumla ya Katoni 500 za taulo za kike zenye thamani ya Sh. Milioni 35.4. Pia imetoa Madawati 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 25.9 kwa shule za tatu za mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu -TEA Bw. Masozi Nyirenda, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano ya Kampuni – TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd, Bi. Getrude Mpangile ameahidi kuwa kampuni yake itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu. Bw. Philipo Silvester Mwalimu Mkuu kutoka Shule ya Sekondari Lemura na Glory Micheal mwalimu wa Shule ya Sekondari Manunus -Mkomboz wamesema msaada huo utasaidia kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wa kike. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *