DKT. MOLLEL ANADI SERA ZA CCM NA KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA UENYEKITI WA MITAA NA VIJIJI

0

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Siha, Dkt. Godwin Mollel, leo ameongoza kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kuhusu umuhimu wa kuchagua wagombea wa nafasi za uenyekiti wa mitaa kupitia chama hicho.

Akizungumza kwenye mikutano mbalimbali iliyofanyika jimboni humo, Dkt. Mollel ametumia fursa hiyo kufafanua mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa CCM, hususan katika Jimbo la Siha akibainisha uwekezaji uliotekelezwa katika sekta za afya, elimu, na miundombinu, akisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa sera thabiti za CCM.

“Tumejenga zahanati, kuboresha shule, na kuimarisha miundombinu ya barabara katika kila kata ya Siha. Mafanikio haya yamewezekana kwa sababu ya uongozi wa CCM. Ninawaomba tuendelee kushirikiana kwa kuwachagua wagombea wetu wa uenyekiti wa mitaa ili kuendeleza juhudi hizi,” amesema Dkt. Mollel.

Aidha, amewataka wananchi wa Siha kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuwapa ushindi wa kishindo wagombea wa CCM. Alieleza kuwa uongozi wa CCM katika ngazi ya mitaa ni muhimu katika kusimamia huduma za msingi na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Siha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *