AWESO ASISITIZA MRADI WA MKINGA-HOROHORO UKAMILIKE KWA WAKATI
Leo tarehe 19 Novemba, 2024 Mhe Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ametembelea Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga na kukagua mradi wa Maji wa Mkinga – Horohoro unaotekelezwa na Mkandarasi STC katika kijiji cha Manza linakojengwa tanki la ujanzo wa mita 300.
Katika ziara hiyo Pamoja na ukaguzi wa mradi huo wenye thamani ya Bil 36 ambao umefikia asilimia 40 ya utekelezaji wake Mhe. Waziri ameagiza kiasi cha fedha Bil 2.6 kilipwe mapema ili kuwezesha utekelezaji wa mradi huo kukamilika mapema ili kuondoka tatizo la maji kwa wakazi zaidi ya 50,000 wanaotegemea kunufaika na mradi.
Aidha Sambamba na maelekezo hayo Aweso ameagiza RUWASA mkoa wa Tanga jitihada za kukamilisha miradi mingine zifanyije ili miradi yote inayoendelea iweze kukamilika kwa wakati na kutoa Msisitizo zaidi kwa wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kwa haraka na uhakika ili ajenda ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani itimie.