DKT. SLAA AIBUKA LISSU NA CHADEMA NI WANAFIKI
Mwanachama Mwandamizi mstaafu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, ameibua unafiki mkubwa ndani ya chama chake cha zamani ukweli ambao umekuwa ukinong’onwa lakini hautamkwi wazi. Ameamua kusema bila kificho kwamba CHADEMA inatamka mambo makubwa, lakini vitendo vyao vinaonyesha picha tofauti kabisa.
Dk. Slaa ameeleza wazi jinsi anavyokerwa na ukimya wa CHADEMA juu ya tuhuma za rushwa zilizotolewa na Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa chama hicho. Katika nafasi yake, Lissu angeweza kutumia madaraka yake kuhakikisha tuhuma hizo zinajadiliwa ndani ya chama na kufanyiwa kazi ili ukweli ujulikane. Lakini kinyume chake, Lissu amenyamaza huku akiwalaghai Watanzania na kauli za uongo dhidi ya CCM na serikali.
Ukweli unaoelezwa na Dk. Slaa ni wa kushtusha: Tundu Lissu na CHADEMA hawatekelezi wanayoyahubiri. Lissu, aliyepata umaarufu kwa kukosoa na kukashifu CCM, ameshindwa kukemea mambo yanayofukuta ndani ya chama chake, ikiwemo rushwa, migongano ya ndani, na unafiki wa hali ya juu.
Kauli za Dk. Slaa ni onyo kwa Watanzania—CHADEMA sio kile wanachodai kuwa. Wanahubiri haki na uwazi kwa umma, lakini ndani ya chama kuna ufisadi, kutupiana vijembe, na usaliti ambao haujasuluhishwa. Kama CHADEMA hawawezi kusafisha nyumba yao wenyewe, vipi wawe na maadili ya kuongoza nchi?
CHADEMA imeshindwa kuonyesha uwajibikaji na uadilifu wa kweli, na Dk. Slaa amefichua unafiki wao kwa ulimwengu. Wanaosema kuwa wanapigania haki na uwazi ni wale wale wanaoificha rushwa na uozo ndani ya chama chao. Wakati umefika kwa Watanzania kuelewa kwamba CHADEMA ni chama kinachokosa dira, na hakiwezi kuaminika kuongoza Taifa letu.