SERIKALI YA TANZANIA HAIJASITISHA UTOAJI WA VISA KWA WAGENI

0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuwajulisha wageni na wadau wote kuwa haijasitisha utoaji wa Visa kwa wageni kwenye vituo vya kuingilia na kutoka nchini.

Hata hivyo, Idara ya Uhamiaji Tanzania inashauri wageni wote ambao wanapenda kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni mbalimbali kuomba Visa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo wa Visa mtandao (e-Visa) https://visa.immigration.go.tz. Kuomba Visa kabla ya kuingia nchini mgeni anakuwa na uhakika wa safari yake na hupunguza msongamano na muda wa kuhudumiwa wakati wa kuingia nchini.

Aidha, Idara ya Uhamiaji Tanzania inawahakikishia kuwa inaendelea kutoa huduma bora zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa kwa wageni wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *