TANZANIA 10 BORA KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA AFRIKA
Tanzania imetajwa kuwa kati ya mataifa 10 bora barani Afrika ambayo yana miundombinu bora zaidi ya barabara.
Taarifa hizi zinakuja ikiwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kuanzia mijini hadi vijijini.
Uwekezaji huo unalenga kuwarahisishia wananchi, kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji kwa urahisi ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa Statista huku ikichapishwa na businessinsider, Tanzania katika 10 bora hizo ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 4.41.