HATIFUNGANI HII INATOKANA NA MPANGO WA KIMKAKATI AMBAO TUNAO KAMA BENKI – DKT. ESTHER

0

“Ninayofuraha na heshima kubwa kuwasilisha waraka wa matarajio wa (hatifungani) wa muda wa kati wenye thamani ya fedha za kitanzania bilioni 100, hatifungani hii inatokana na mpango wa kimkakati ambao tunao kama benki wa miaka mitano ambao ulianza mwaka jana 2023 mpaka 2027.

Matarajio yetu fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya hatifungani hii zitatumika katika sekta mbalimbali za uchumi ikiwa jitihada za kushirikiana na serikali katika kutekeleza ajenda za maendeleo ya nchi yetu.

2023 ulikuwa mwaka wa kwanza wa utekelezaji wetu wa mpango mkakati wa benki yetu, na benki ilifanikiwa kupata matokeo mazuri, tulikuza mezania kufika trilioni 2.3 na kutengeneza faida ya bilioni 29 na kutangaza gawio la bilioni 8 kwa wana hisa.

Benki yetu ina matawi makubwa 25, matawi madogo 11, maduka ya kubadilisha fedha 7, ATM 36 na mawakala zaidi ya 5000, mheshimiwa mgeni rasmi hatifungani hii itatolewa kwa awamu mbalimbali itakuwa hatifungani ya kipekee sokoni yenye muda wa miaka minne na riba 12.5%, itakuwa inalipwa kila baada ya miezi mitatu, huu ni upekee wa hatifungani hii inayoitwa Bondi yangu.

Fedha itakayopatikana inategemea kuwanufaisha watanzania wengi kutoka makundi mbalimbali ikiwemo makundi ya wanawake na vijana.” Dkt. Esther Mang’enya Mkurugenzi mtendaji wa Azania Bank akisoma waraka mbele ya mgeni rasmi Dkt. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya Best western jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *