MWIGULU ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA SHIRIKA LA FEDHA MAREKANI

0

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania, katika Mkutano wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( @the_imf ) wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group I Constituency) uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Mkutano huo ulijadili masuala ya kiutawala na namna ya nchi wanachama za Ukanda huo wa Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto za athari hasi za mabadiliko ya tabianchi na kukuza Uchumi kwa kushirikiana na Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani.

Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila, na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *