JELA MIAKA 3 KWA WIZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI DODOMA

0


Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemhukumu Bwana Enock Mwalimu kifungo cha miaka mitatu na siku saba kwa kosa la wizi wa miundombinu ya maji na kujifanya Mtumishi wa Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 23, 2024 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Nyamburi Tungaraja.

Akitoa taarifa kwa Umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Ayoub Mganda amesema DUWASA inatoa siku kumi na tano kuanzia Oktoba 23, 2024 kwa wateja wanaodaiwa kulipa madeni yao kabla Sheria haijachukua mkondo wake.



Tayari DUWASA imewafikisha wateja thelathini wenye madeni Sugu Mahakamani wanaodaiwa zaidi ya shilingi milioni 30.

Aidha, Mkuu huyo wa Kitengo cha Sheria DUWASA amewataka wananchi kulinda na kutoa taarifa ya uharibifu wa miundombinu ya maji pale wanapoona inahujumiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *