TANZANIA NA HUNGARY KUSHIRIKIANA KATIKA KUBORESHA SEKTA YA MAJI NCHINI

0

Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng Mwajuma Waziri wamekutana na Balozi wa Hungary mwenye makazi yake Nairob Kenya Mh.Zsolt Meszaros akiwa na ujumbe kutoka Hungary.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za DAWASA Dar Es Salaa kimelenga kupanua wigo wa Mashirikiano na Serikali ya Hungary hususani katika sekta ya Maji.

Aidha, Mheshimiwa Balozi ameeleza ya Kwamba nchi yake inatoa mikopo isiyokuwa na riba kupitia programu ya Hungarian Tied End Credit, l Balozi Zsolt akifafanua zaidi amesema kupitia programu hiyo Tanzania itanufaka eneo la uwekezaji kwenye sekta ya Maji.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemueleza Balozi ya kuwa Wizara ya Maji ipo tayari Kwa ajili ya Mashirikiano katika kuhakikisha lengo la kumtua Mama ndio kichwani linatimia kwani ndio kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *