DKT. TULIA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 5 Oktoba, 2024 alipokuwa Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Beyora Mission iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo amesema kuwa hatua hiyo imeongeza chachu ya kukuza na kuhamasisha jamii kuipenda elimu.

Aidha, alielezea juhudi hizo ambazo zinajumuisha ongezeko la bajeti ya elimu hadi kufikia shilingi trilioni 1.96 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ujenzi wa madarasa 15,000 nchi nzima, kuongeza udahili wa wanafunzi, kuendelea kutoa elimu bila ada, kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza ajira kwa walimu na kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Sambamba na hayo, Dkt. Tulia amewapongeza Walimu wote nchini kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele katika uadilifu wa kutekeleza majukumu yao ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi nchini ili kufanikisha malengo ya Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *