HATMA YA MAKAMU WA RAIS KENYA KUFAHAMIKA LEO

0

Muswada wa kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua madarakani utawasilishwa Bungeni leo, Oktoba 1, 2024, Saa 8:30 Mchana. Ikiwa Muswada huo utapitishwa, Spika wa Bunge, Moses Wetangula atawasilisha uamuzi huo kwa Spika wa Seneti Amason Kingi kwa hatua zaidi

Gachagua anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Rais William Ruto, huku akikabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi, kufadhili fujo za Gen Z katika Maandamano, kutoa siri za Serikali na Kuchochea Ukabila

Gachagua ametoa onyo kwa Rais Ruto, akisema kwamba kama Washirika wake wataendelea na hoja ya kumwondoa, Ruto anaweza kupoteza uungwaji mkono wa eneo la Mlima Kenya. Amehimiza uongozi wa Ruto kutulia na kuruhusu serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *