PICHA: UZINDUZI WA SHULE YA WASICHANA YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa ya Dkt.. Samia Suluhu Hassan iliyopo katika kitongoji cha Migeregere kata ya Rwinga, Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma tarehe 27 Septemba, 2024.

Shule hii ni miongoni mwa shule 26 za Wasichana za Sayansi za Mikoa zilizojengwa kwenye Mikoa yote Tanzania bara na imejengwa kwa gharama ya shilingi Bil. 4.6 ikiwa vyumba vya madarasa 22, mabweni 8, nyumba za walimu 3 (2 in 1), Nyumba ya Mkuu wa shule, Nyumba ya Matron, chumba cha TEHAMA, Maktaba, Jengo la Utawala pamoja na uzio upande wa Mabweni.

Shule hii ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200 na mpaka sasa wanafunzi waliopo ni 548.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *