RC SINGIDA ABORESHA TAARIFA ZAKE KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego akionesha Kadi yake ya Mpiga Kura baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloanza Uboreshaji Septemba 25,2024 na litadumu kwa siku saba mkoani Singida hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa aliboresha taarifa zake katika Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25,2024.
Akizungumza baada ya kumaliza uboreshaji, Mhe.Dendego aliwahimiza wananchi wa mooa wa Singida kujitokeza kwa wingi kujiandikisha lakini pia kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati huu ambao Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeweka kambi mkoani humo.
Amesema ni muhimu kila mwanasingida mwenye Sifa kujitokeza na kujiandikisha ili apate fursa ya kujiandikisha katika Daftari hilo ili apate fursa ya kuchagua viongozi anaowataka wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kushoto) akiangalia kadi ya Mpiga Kura aliyokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego mara baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Wapiga Kura katika uboreshaji ulioanza jana mkoani Singida.Wananchi wa Mkoa wa Singida wameanza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (katikati) akishudia Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akichukuliwa taarifa zake na Mwandishi Msaidizi Failuna Bira wakati mkuu huyo wa mkoa alipofika katika Kituo cha Chuo cha ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba,Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida. Wananchi wa Mkoa wa Singida wameanza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (kulia) akichukuliwa picha na Mwendesha Vifaa vya Biyometriki (BVR), Christina Isaya aliyepo Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25,2024 katika siku ya kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Singida. Katikati ni Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (kushoto) akiweka saini katika kadi yake ya Mpiga Kura kupitia kishkwambi cha BVR. Mkuu wa Mkoa aliboresha taarifa zake katika Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea vituo kadhaa na kushuhudia wananchi mbalimbali wakijiandikisha na kuboresha tarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Uboreshaji wa Dafrati la Kudumu la Wapiga Kura umeanza leo Septemba 25, 2024 na utadumu kwa siku sana hadi Oktoba 1 mwaka huu.
Wananchi wakiwa katika vituo vya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari hilo mkoani Singida.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea vituo kadhaa na kushuhudia wananchi mbalimbali wakijiandikisha na kuboresha tarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.