RAIS SAMIA ASEMA WAZIRI WA MAJI NA KATIBU MKUU WAKE NI WACHAPAKAZI, AWAPA MIEZI 3 WANANCHI WAPATE MAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng Mwajuma Waziri ni wachapakazi sanana wanafanya kazi nzuri hivyo kuwapa miezi mitatu kuhakikisha maji yanapatikana ndani kwa wakazi wa Mtyangimbole kwani tayari mradi huo umefikia asilimia 50% na wananchi wana matumaini makubwa sana.
Mradi huo uliogharimu kiasi cha Bilion 5.5 na utakaohudumia wananchi zaidi ya elfu kumi na nne umewekewa jiwe la msingi na Mhe Rais Samia leo tarehe 24 Septemba 2024 kwa niaba ya miradi 30 inayoendelea kutekelezwa vijijini Mkoani Ruvuma.
//
To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025
Sign Up for Our Newsletter
Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!
Email address:
© 2024 MILLARD AYO. All Rights Reserved. Designed by Ayo.