JIMBO LA PERAMIHO-RUVUMA KUFIKIA ASLIMIA 85% UPATIKANAJI WA MAJI – AWESO

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika jimbo la Peramiho umefikia Asilimia 73 ambapo bado Kuna miradi inaendelea ikiwemo mradi wa maji Kizuka, Lipaya, Lipokela ya zaidi ya Bilioni 4 ambapo mara baada ya kukamilika kwa miradi hii upatikani wa huduma ya maji utafika zaidi ya asilimia 85.

Mhe. Aweso ameyasema hayo leo Septemba 24 ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati aliposimama na kusalimiana na wananchi wa Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma.

Aidha Mhe. Aweso amemtaka mkandarasi ahakikishe anamaliza miradi hiyo kwa wakati ili wananchi waendelee kunufaika na fedha nyingi zinazotolewa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine Mhe. Aweso amemuhakikishia Mbunge la Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama kuwa kupitia programu ya uchimbaji wa Visima vijiji vyote vitaenda kupata Majisafi na Salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *