NAIBU WAZIRI MHE.SANGU AVIPIGIA CHAPUO VIKUNDI VYA TASAF MIKOPO YA HALMASHAURI

0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu amezielekeza Halmashauri Mkoani Tabora kutoa kipaumbele kwa vikundi vya akiba na mikopo vinavyoundwa na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika utoaji wa mikopo.

Mhe. Sangu ametoa maelekezo hayo leo alipokuwa akitembelea miradi ya TASAF katika Kata ya Ipuli wilayani Tabora mkoani humo.

Amesema vikundi hivyo vinastahili kupewa mikopo kwa kuwa vimepewa elimu ya ujasiriamali kupitia TASAF na vimehakikishwa kuwa na nidhamu katika ukopaji na ulipaji.

Amefafanua kuwa mikopo ya asilimia kumi ambayo hutolewa na Halmashauri kote nchini huku akizitaka Halmasjauri hizo zifanye kazi kwa kushirikiana na TASAF ili zijifunze jinsi ilivyofanikiwa katika suala la utoaji mikopo kwa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana

Amesema TASAF inasaidia walengwa wake kuanzisha na kuendesha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana na kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ii kukuza uchumi wa kaya zao.

Akizungumzia mpango wa Ajira za muda kwa Walengwa, Mhe. Sangu amesema kuwa mpango huo si tu unatoa ujira na kusaidia kupunguza umaskini, bali pia ni fursa kwa walengwa kujifunza ujasiriamali na ufundi ambao huwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Hata hivyo Mhe. Sangu amepiga marufuku utaratibu wa kazi za ajira za muda kwa makundi yafuatato ikiwemo wazee wenye zaidi ya miaka 65 na kuendelea, watoto chini ya miaka 18 na akina mama wajawazito pamoja na watu wenye ulemavu.

Aidha, Mhe.Sangu amezitaka kaya za walengwa ambazo zina vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wana vigezo vya kujiunga na masomo ya elimu ya juu kutoa taarifa TASAF ili wapewe barua kwa uambatanisha na maombi ya mkopo ili aweze kupata mkopo huo kwa asilimia 100.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha amesema ujio wa TASAF katika Mkoa wake imeleta mapinduzi makubwa kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo wanufaika 13,467 wamewezeshwa kujiunga na Bima ya Afya Iliyoboreshwa (CHF), kuboresha makazi na kuanzisha vikundi vya kukopeshana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *