AWESO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA VISIMA 5 KILA JIMBO TUNDURU

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameweka jiwe la Msingi mradi wa uchimbaji Visima 5 kwa kila Jimbo katika Kijiji cha Azimio kata ya mtina Wilaya ya Tunduru na kushuhudia zoezi la usafishaji wa Kisima Kimoja (Flushing) kitakacho wahudumia takribani wananchi 3427 wa kijiji hicho

Akizungumza na wananchi wa Azimio katika Mhe. Aweso amewahakikishia kuwa Serikali ya Dkt. Samia imejipanga kumaliza changamoto ya maji katika vijiji vyote nchini ambapo amewaelekeza wataalam wa Wizara kufanya usanifu wa Mradi katika kijiji hicho huku akibainisha ndani ya siku 7 ataleta fedha Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi huo

Awali akitoa Salamu Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini uchimbaji wa kisima  wilaya ya Tunduru jimbo la tunduru kusini Mhe. Idd Mpakate ameishukuru serikali kwa kuanzisha programu ya uchimbaji wa Visima 5 katika kila Jimbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *