RAIS SAMIA ATOA MILIONI 425 UJENZI NA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA KIJAMII LONGIDO.

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ametoa takribani Shilingi Milioni 425 kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Huduma za Kijamii kwenye Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa, ambaye anaendelea na ziara yake Mkoani Arusha akianzia kwenye Wilaya hiyo ya Longido iliyo Mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Katika Mgawanyo wa fedha hizo, Shilingi Milioni 300 zimeelekezwa kujenga Kituo cha afya Matiani, huku Fedha nyingine zikielekezwa kwenye ujenzi wa Daraja pamoja na ukarabati wa Barabara inayounganisha Kata ya Matiani na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.

Katika Hatua nyingine Mhe. Mchengerwa akijibu hoja na Kero mbalimbali za Wananchi, Waziri Mchengerwa ameielekeza wizara ya TAMISEMI kuandaa tuzo na cheti maalum cha shukrani na pongezi kwa Mzee Lekule Laizer kutokana na mchango wake mkubwa katika kuharakisha maendeleo ya Longido alipokuwa Kiongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, serikali na Bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *