WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA MAJI BONDE LA RUHILA WALIPWA FIDIA

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amekabidhi Hundi ya Kiasi cha Shilingi Milioni 925,333,158.00 ikiwa ni fidia kwa wananchi walipisha Mradi wa Maji Bonde la Ruhila linalotegemewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea kwa ajili ya kuwahudumia wananchi huduma ya Maji ambapo haya ni maelekezo yaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Waziri Aweso Amekabidhi hundi hiyo wilayani Songea akiendelea na Ziara yake Mkoani Ruvuma ya kutembelea na Kugagua utekelezaji wa Miradi na hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji mkoani hapo.

Akizungumza na Wananchi Mhe. Aweso amewataka watandaji wa Wizara kuhakikisha baada tu ya kukabidhi hundi malipo hayo yaaanze kufanyika haraka ili wananchi wanufaike na fedha hizi zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maji.

Awali Mbunge wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye ndio Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ameishukuru serikali ya Dkt. Samia kwa kuwajali wananchi wake ambapo amebainisha kuwa mpaka sasa Jumla ya Shilingi Bilioni 2.8 zimeshatolewa kama fidia kwa wananchi walioathiriwa na Mradi wa Bonde la Ruhila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *