BREAKING: DIDDY ARIPOTIWA KUKAMATWA

0

Rapper maarufu Nchini Marekani ambaye pia ni Producer na Mfanyabiashara Sean ‘Diddy’ Combs ameripotiwa kukamatwa na Mamlaka Nchini humo akiwa Jijini New York, akikabiliwa na mashtaka kadhaa ambayo bado hajawekwa wazi.

Diddy amekamatwa katika eneo la Manhattan Nchini humo baada ya kuzingirwa kwa makazi yake ya Los Angeles na Miami ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea, mitandao ya AFP, The New York Times, CNN ,TMZ na mingine Nchini Marekani imeripoti.

Diddy amekamatwa ikiwa imepita miezi kadhaa tangu EX wake ambaye ni Mwimbaji Cassandra Ventura (Cassie) alipofungua kesi akimtuhumu Diddy kwa ubakaji na unyanyasaji kipindi chote cha mahusiano yao yaliyoanza miaka 20 iliyopita na baadaye Jumba la kifahari la Diddy likazingirwa mwezi March mwaka huu na Maafisa wa usalama ambao ilidaiwa walipanga kumkamata Diddy lakini hata hivyo hawakufanya hivyo.

Mwanasheria wa Diddy, Marc Agnifilo amesema amesikitishwa na kukamatwa kwa Diddy na kusema Mteja wake huyo ni Mtu mwema asiye na hatia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *