MAANDAMANO YA CHADEMA YAPIGWA MARUFUKU, JESHI LA POLISI LATOA TAMKO

0

Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo na kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa na Viongozi wa CHADEMA September 23,2024 na kusema Mtu yeyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Nchi.

Akiongea Mjini Moshi leo September 13,2024, Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “September 11,2024 kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii walisikika Viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho (Freeman Mbowe), akiwahamasisha Wakazi wa Dar es salaam kuingia barabarani kuanzia September 23,2024, Viongozi hao waliendelea kuhamasisha Wananchi wa Kanda mbalimbali Nchini kukutana Dar es salaam ili kuungana na Wakazi wa Dar es salaam kuingia barabarani”

“Hatua hiyo waliyofikia tunajiuliza na tunaendelea kufuatilia na kuchunguza kwanini wanataka kututoa kwenye reli ya hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia kuviagiza Vyombo vya Uchunguzi vifanye uchunguzi kisha wawasilishe uchunguzi kwake”

“Ikumbukwe mara kadhaa Viongozi na Wafuasi wa Chama hicho wamekuwa wakipanga, kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa matamshi yenye lengo la kuleta vurugu Nchini ili kuharibu amani ya Nchi yetu kwasababu wanazozijua wenyewe”

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa Viongozi wa Chama hicho kuacha kuendelea kuhamasisha Wananchi kujihusisha katika uhalifu huo na yoyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Nchi, kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku, naomba kurudia kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku”

“Jeshi la Polisi linatoa katazo kwa yoyote aliyealikwa, kuelekezwa kufika Dar es salaam kutoka Mkoa wowote ule kwa ajili ya maandamano hayo asithubutu kufanya hivyo kwani maandamano hayo ni haramu na hayatofanyika hivyo asipoteze muda na gharama zake, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi wapenda amani kutokubali kurubuniwa, kudanganywa au kushawishiwa kwa namna yoyote ile kushiriki kwenye maandamano hayo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *