CCM HAUSIKI NA UTEKAJI NCHIMBI AFUNGUKA

0

Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi amesema CCM haihusiki na utekaji na mauaji yanayoendelea Nchini bali vitendo hivyo vinafanywa na magenge ya uhalifu yenye nia ya kufarakanisha Taifa na kuikosanisha CCM na Wananchi.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Nchimbi amesema “Siku chache zilizopita Kiongozi wa CHADEMA alitekwa na kuuawa kikatili na jambo sio dogo limepata Wazungumzaji wengi tukaona na Mimi nilisemee, Ilani ya CCM ukurasa wa 156 inasema moja ya mambo tutakayofanya ni kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti usalama wa Raia na mali zao”

“Mtu yoyote anayeshiriki kuteka Raia au mauaji ya Raia ni wazi wanajua wanafanya hivyo ili kuharibu taswira ya CCM mbele ya Umma na ndio maana kama ni Mtu au genge la Watu linajihushisha na kuteka Watu au kuua Watu haliwezi kuwa na nia njema na CCM”

“Ni Mwendawazimu pekee yake anaweza kutamka kwamba CCM inaweza ikafanya jambo la kujiumiza yenyewe kwasababu CCM sio Chama cha Watu Wajinga, ni Chama cha Siasa kisichojitambua ambacho kinaweza kufanya matendo ya kufanya kikosekane na Wananchi wake, Watu wenye nia mbaya ndio wanaoendesha magenge ya uhalifu Nchini ili kukikoseshanisha Chama chetu na Wananchi na kufarakanisha Taifa, ni Watu hawa wanasababisha Watu wenye busara sana waongee maneno yasiyotarajiwa”

“Tumemsikia Mbowe akitoa muda wa mwisho wa Serikali kuwataja Wahusika wa matendo hayo maovu na akisema ikifika Sept 23,2024 hawajatajwa watachukua hatua, kwa Mbowe ambaye nakiri ni Rafiki yangu mwenye hekima kubwa akiwa amefikishwa hapo na genge la Watekaji kwa Mbowe kutoa muda wa mwisho kwa Rais, ukifikishwa hapo ujue genge la Watekaji limefanikiwa, tunatakiwa sisi na upinzani kushirikiana kuhakikisha genge la Watekaji halifanikiwi kutufarakanisha, kosa kubwa tutakalofanya ni kuwapa ushindi genge la Watekaji” Dr. Nchimbi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *