ZAIDI YA TRIL 1.8 ZACHANGIWA NA KAMPUNI ZA MADINI , MAFUTA NA GESI ASILIA TANZANIA

0

Imeelezwa kwamba zaidi ya shilingi trilioni 1.8 zilichangiwa na Kampuni zinazojishughulisha na sekta ya Uziduaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini.

Hayo yalibainishwa na waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa akizindua ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa Mwaka wa Fedha wa 2021/22.

Waziri Mavunde alisema kuwa ripoti hiyo inaonyesha mchango wa sekta hizo kwa jamii ambapo amewataka wadau wa maendeleo kutumia takwimu zilizopo katika ripoti hiyo katika mijadala, warsha na makongamano mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi hususani katika sekta husika.

Akielezea kuhusu ulinganisho wa mapato kutoka katika Kampuni, Waziri Mavunde alieleza kwamba ripoti hiyo inaonesha ulinganisho wa mapato kutoka katika kampuni 44, ambapo Kampuni 26 za Madini, Kampuni 7 za Gesi Asilia na Kampuni 11 za Utoaji huduma kwenye mnyororo mzima wa thamani Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Akifafanua kuhusu mafanikio ya Mpango wa Ushirikishwaji wa Jamii katika utoaji huduma migodini, Waziri Mavunde ameeleza kuwa katika Mwaka wa Fedha 2023/24 kiasi cha shilingi trilioni 3.1 zilitumika kwenye manunuzi ya bidhaa na utoaji huduma katika sekta ya Madini.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. Mathayo David Mathayo aliipongeza kamati ya TEITI kwa kazi nzuri ikiwa pamoja na kuweka kipaumbele cha Uwazi na Uwajibikaji kwenye mapato yatokanayo na Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa manufaa ya Taifa.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo, alipongeza TEITI kuwa Taasisi rasmi inayojisimamia katika masuala ya Uziduaji ambapo kupitia ripoti zake inajibu maswali mbalimbali kwa jamii na wadau husika yanayohusiana na Uziduaji kwenye sekta ya Madini , Mafuta na Gesi Asilia.

Awali, akielezea kuhusu mwenendo wa utoaji ripoti na mafanikio yake , Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Ludovick Utouh amesema kuwa, mwezi Novemba 2023, Bodi ya EITI iliwasilisha ripoti ya kuonesha kuwa Tanzania imeingia daraja la tatu kwenye kutekeleza viwango vya Kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *