WAZIRI SILAA AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND NCHINI TANZANIA, THERESA ZITTING

0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (Mb.), amekutana na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Theresa Zitting, aliye ambatana na Balozi Mdogo wa ubalozi huo, Bw. Tomi Lounio, leo Septemba 12, 2024, katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mbalimbali yahusuyo TEHAMA na Mawasiliano, ikiwa ni pamoja na Mashirikiano katika Usalama wa Mtandao, Miundombinu ya TEHAMA, Akili Mnemba (Artificial Intelligence), pamoja na Kubadilishana uwezo katika Uchumi wa Kidijitali na Mifumo ya TEHAMA.

Pamoja na masuala tajwa hapo juu, Serikali ya Tanzania na Finland zinashirikiana kwenye kubadilishana uzoefu na teknolojia katika kutumia njia bora za kuhakikisha Mifumo ya TEHAMA hapa nchini inasomana ikiwa ni mojawapo ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa la kuhakikisha ifikapo mwezi Disemba, 2024 Mifumo ya TEHAMA iwe inasomana. Finland ndio Nchi inayoongoza Duniani kwenye Uchumi wa Kidijitali.

Wengine waliohudhuria kikao hiki ni Bw. Mohamed Mashaka – Mkurugenzi wa Uendelezaji Mifumo na Huduma za TEHAMA, Mhandisi Leo Magomba – Mkurugenzi wa Miundombinu ya TEHAMA – Ahmed Kaubebe, Msaidizi wa Waziri na Bertha Mturi – Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *