TYLA LAURA ASHINDA TUZO MTV VIDEO MUSIC AWARDS

0

Mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Tyla Laura Seethal maarufu Tyla ameshinda tuzo ya MTV Video Music Awards (VMA) 2024 katika kipengele cha ‘Best Afrobeat’ kutokana na wimbo wake wa ‘Water’.

Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika nchini Marekani, Tyla alianza kwa kutoa shukrani na kusema ulikuwa wakati mzuri kwa muziki wa Afrika.

Amesema ushawishi wa wimbo wake maarufu duniani kote ni ushahidi kwamba muziki wa Kiafrika unaweza kuwa muziki wa pop pia.

Mwanamuziki huyo aliendelea kuzungumzia muziki huo wa Kiafrika kwa kusema
“Hii ni maalum sana, lakini pia ni tamu na chungu kwa sababu najua kuna tabia ya kuwapanga wasanii wote wa Kiafrika chini ya Afrobeat”.

Tyla aliendelea kwa kusema kuwa anatokea Afrika Kusini na anawakilisha utamaduni wake, huku akihitimisha kwa kuwapongeza wanamuziki wa Afrobeats ambao waliteuliwa katika kipengele alichoshinda akisema ‘nawapenda’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *