KAKA WA POGBA KUSOMEWA MASHTAKA YA UTAPELI NA ULAGHAI NA WENGINE 5

0

Mathias Pogba, kaka wa Mshindi wa Kombe la Dunia Paul Pogba, atafikishwa Mahakamani pamoja na Wanaume watano katika kesi ya ulaghai iliyoelekezwa kwa Mchezaji huyo miaka miwili iliyopita.

Aidha Ofisi ya mwendesha mashtaka ilitangaza kuwa Mathias atashtakiwa kwa jaribio la ulaghai na njama za uhalifu, hata hivyo, tarehe ya kesi bado haijatangazwa.

Washukiwa hao walidai Dola milioni 14.3 kutoka kwa Pogba huku wakimtishia mara kwa mara, Kundi hilo linatuhumiwa kwa kufanya vurugu, utekaji nyara, na kumfunga Pogba ili kuwezesha ulaghai huo, na wakati wa uchunguzi, Pogba alikiri kulipa Dola 70,000 kwa kundi hilo, akiwemo kaka yake.

Kesi hiyo ilijulikana hadharani mwezi Agosti 2022 baada ya Mathias kuposti video kwenye mitandao ya kijamii, akidai kuwa angefichua taarifa za kushtua kuhusu kaka yake Paul, wakala wake Rafaela Pimenta, na Mchezaji mwenzake Mbappé.

Mathias Pogba alikamatwa kwa muda mfupi, akiwa pia Mchezaji wa timu za madaraja ya chini barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *