DK. BITEKO ATETA NA ABIRIA NDANI YA TRENI YA SGR

0

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko amesafiri kwa treni ya mwendokasi maarufu kama SGR, asubuhi ya leo akitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma huku akitumia muda wake kuwasikiliza abiria waliosafiri naye katika treni hiyo.

Dk. Biteko alipita katika mabehewa mbalimbali ya treni hiyo na kusikiliza maoni ya baadhi ya abiria huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kusimamia vyema mradi huo ili uweze kuleta manufaa makubwa kiuchumi kwa nchi na wananchi mmoja mmoja.

Naibu Waziri Mkuu pia amesema umeme unaotumika kuendesha treni hiyo ni wa uhakika kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa nishati hiyo hivyo wananchi hawapaswi kuwa na hofu yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *