RAIS SAMIA AIPONGEZA TAIFA STARS

0

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa Stars kufuatia ushindi walioupata Ugenini dhidi ya Guinea siku ya jana (2-1). Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii ameandika;

“Hongera kwa vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi wenu dhidi ya Guinea katika hatua ya makundi kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Tunawaunga mkono na kuendelea kuwatakia kila la kheri katika hatua hii muhimu”

Mchezo huo umeiweka Stars katika nafasi nzuri ya kufuzu katika michuano ya AFCON 2025, wakiwa na Alama 4 nyuma ya vinara wa kundi DR Congo wakiwa na alama 6, huku Ethiopia wakiwa na alama 1 na Guinea wakiburuza mkia wakiwa na alama 0.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *