DKT. TULIA AWASILIA JIJI YA YEREVAN NCHINI ARMENIA

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 11 Septemba, 2024 amewasili Jijini Yerevan nchini Armenia ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa 10 wa Wabunge Vijana wa IPU utakaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 11 hadi 15 Septemba, 2024.

Dkt. Tulia amepokewa na Mhe. Arsen Torosyan ambaye ni Mbunge na Mwakilishi wa Bunge la Armenia kwenye IPU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *