KAMPUNI YA APPLE YAZINDUA AINA MPYA YA SIMU ZA MKONONI

0

Kampuni ya Apple inayotengeneza bidhaa mbalimbali za kiielektroniki imezindua aina mpya za simu za mkononi ambazo ni iPhone 16, iPhone 16 Plus, iPhone 16 Pro na iPhone 16 Pro Max.

Simu hizo mpya ni kubwa zaidi ya matoleo mengine zikiwa zimewekewa kamera yenye uwezo mkubwa na kupiga picha ang’avu huku zikitumia teknolojia ya A18 Pro.

Taarifa za kampuni hiyo zinaonesha kuwa simu hizo zimepewa uwezo wa juu kufanya utambuzi na pia kufungwa vifaa vinavyoendana na teknolojia za kisasa za matumizi ya simu za mkononi.

Simu hizo zimetofautiana kwa rangi tofauti na matoleo mengine ya simu za iPhone ambapo simu hizo mpya zina uwezo wa kupiga picha Jongefu (Video) kwa ubora wa 4K120

Hili ni toleo la 16 kwa simu zinazotengenezwa na kampuni ya Apple na kwa mara ya kwanza kampuni hiyo imetoa matoleo manne kwa wakati mmoja ya simu za iPhone 16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *