AWESO AMTENGUA MKURUGENZI MAMLAKA YA MAJI CHATO KISA ULEVI
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesikitishwa na tabia ya isiyo njema ya kinidhamu ya ulevi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Chato Eng.Mari Misango ambaye amefika kwenye mkutano wake leo akiwa katika hali ya ulevi na kwa ujumla akiwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake vyema kutokana na kukithiri kwa tabia hii na kulalamikiwa na watumishi anaowaongoza katika Mamlaka ya Maji Chato.
Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri kumuweka pembeni katika nafasi ya uongozi Bwana Misango na ametuma salamu kwa watendaji wote wa sekta ya Maji nchini kuzingatia Nidhamu katika kazi kwani sekta hii ji sekta ya huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemteua Eng. Isaack Joseph Mgeni kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji ya Chato ambapo awali a Eng. Isaack aliekua Meneja wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Maji Geita (GEUWASA)
Waziri Aweso amefanya maamuzi haya alipotembelea Mradi wa Maji wa Miji28 wa Chato unaogharimu kiasi cha Bilion 38 baada ya Maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi na kusisitiza mradi huu unahitaji uangalizi wa karibu.