RAIS SAMIA NIMEAGIZA VYOMBO VYA UCHUNGUZI KUNILETEA TAARIFA YA KINA TUKIO HILI, MAUJI YA KIONGOZI WA CHADEMA

0

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *