KITUO KITAPOKEA MALALAMIKO BILA MWANANCHI KUFIKA WIZARANI-PROF. KABUDI

0

Wizara ya Katiba na Sheria imeanzisha Kituo cha Huduma Kwa Mteja kwa Huduma za kisheria baada ya kubaini kuwa malalamiko mengi ya wananchi yamekuwa yakiwasilishwa wizarani kwa njia ya Barua au kufika moja kwa moja kwenye Ofisi za Wizara kwa kutumia gharama kubwa.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kituo hicho leo Septemba 05, 2024 Mtumba Jijini Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi

Kabudi amesema uwepo wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambayo inaendeshwa na Wizara katika maeneo mbalimbali nchini imeleta hamasa kubwa ya wananchi kuwasilisha malalamiko na hoja mbalimbali za kisheria ambazo zinahitaji ufumbuzi wa haraka

Kituo hicho kitawezesha kupokea Taarifa na malalamiko yanayohusu tuhuma za rushwa, ukiukwaji wa haki unaofanywa na Taasisi ama mtu mmoja mmoja, na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusiana na huduma zinazotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria, pamoja na Taasisi zote zilizo katika mnyororo wa haki.

“kupitia Huduma hii, sasa wananchi walioko mbali wanaweza kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya simu katika Kituo cha Huduma Kwa mteja na malalamiko hayo yatafanyiwa kazi Kwa wakati bila Mwananchi kulazimika kufika Ofisi za Wizara” Amesema Waziri Prof. Kabudi.

Aidha, hadi kufikia 31, Agosti 2024 jumla ya malalamiko 499 yamesajiliwa, kati ya hayo 410 sawa na asilimia 82 yamefanyiwa kazi Kwa ukamilifu.na 89 ambayo ni asilimia 18 yako katika hatua mbalimbali za kutafutiwa ufumbuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *