MAHAKAMA YAAMURU AZAM MEDIA KUMLIPA BONDIA MWAMAKULA MIL. 250

0

Bondia Mtanzania Amosi Mwamakula ametakiwa kulipwa Fedha za Kitanzania Tsh. Milioni 250 na Kampuni ya Azam Media Limited baada ya kushinda Kesi katika Mahakama ya Kinondoni Jijini Dar es salam.

Kesi hiyo ya Madai iliamuliwa 22 Agosti, 2024 na Hakimu William Kaaya kwa Kosa la Kampuni hiyo kufanya Uvunjifu wa Haki Miliki ambapo Bondia huyo aliwadai Azam Media Limited na Patrick Kahemela waliiba wazo la Boxing KAZI KAZI na kuliita Vitasa.

Kwa mjibu wa Taarifa ni kuwa, Boxing Kazi Kazi ni vipindi vya Boxing na Proposal ambayo ilisajiliwa Cosota mnamo Mwaka 2017, na Vitasa ikaja kusajiliwa Mwaka 2021 huku Proposal hiyo na Vipindi Bondia huyo alivituma Kwenye Barua Pepe (email) ya Patrick Kahemela ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi wa Michezo Azam Media Limited na baada ya kupokea alimthibitishia kuwa awe mvumilivu itakapofika 2020 atampa nafasi.lakini baada ya Mwaka mmoja alianza kuona Maudhui hayo yakiruka hewani kwenye Television.

Baada ya hapo Bondia Mwamakula alipeleka Shtaka lake Cosota na wakifanya Kikao Cha Usuluhishi na kuamua kuwa Boxing KAZI KAZI pamoja na Vitasa ni mawazo mfanano ndipo Mdai aliamua kwenda Mahakamani ili kupata Stahiki zake za msingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *