TANZANIA YAZIDI KUNG’ARA FEASSA 2024
Timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya shule za msingi na sekondari kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA 2024) zimeendelea kufanya vizuri katika michuano hiyo inayoendelea nchini Uganda.
Katika mchezo wa soka la wasichana, Tanzania imetawazwa kuwa bingwa baada ya kujikusanyia pointi 11, baada ya kushinda mechi tano na kutoka sare michezo miwili wakati kwa soka la wavulana Tanzania imeshika nafasi ya pili baada ya kupata pointi 6 baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi tano.
Kwa upande wa mchezo wa netiboli, Tanzania imeshika nafasi ya pili baada ya kuichapa wenyeji wa michuano hiyo Uganda kwa magoli 44-31 katika mchezo ambao ulikuwa unamua nani ashike nafasi hiyo baada ya timu hizo kufungana kwa pointi.
Mchezo huo uliocheza kwenye viwanja vya shule ya msingi Bukedea ulikuwa wa vuta ni kuvute, lakini umahiri wa wachezaji wa Tanzania uliwawezesha kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 35-21.
Mbali na matokeo hayo, tayari Tanzania imetawazwa kwa mara nne mfululizo kuwa bingwa wa michuano hiyo kwa upande wa mchezo wa mpira wa goli ambao uchezwa na wanafunzi wenye huoni hafifu.