DKT. MPANGO AILEKEZA WIZARA YA MADINI KUSIMAMIA MADINI MKAKATI KWA MANUFAA YA WATANZANIA

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Madini kuhakisha inasimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

Mh. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Katika eneo La Mpwayungu,Wilaya ya Chamwino-Dodoma wakati akihitimisha ziara ya siku 4 ya Mkoa wa Dodoma.

“Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimalo hii ya madini mkakati yenye mahitaji makubwa sana Duniani.

Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini haya mkakati kwa uwingi na aina tofauti tofauti,lazima rasilimali hii ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

Wizara ya Madini hakikisheni mnaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hii kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo”Alisema Dkt. Mpango

Akiwasilisha salamu za Wizara,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amemuahidi Dkt. Mpango kuyafanyia kazi maelekezo yote na kwasasa Wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini haya ili yalete faida kwa nchi kwa kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini.

Mh. Mavunde alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Afisa Madini Wakazi(RMOs) kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maeneo yenye uchimbaji wa madini mkakati ili manufaa yake yaonekane kwa Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *