DKT. TULIA AFUNGUA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA BUNGE LA CHINA

0

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 20 Agosti, 2024 amefungua maadhimisho ya miaka 40 ya Uanachama wa Bunge la Watu wa China kwenye IPU katika Ukumbi wa Bunge hilo Beijing, China.

Katika maadhimisho hayo yanayoambatana na semina elekezi kwa Mabunge ya nchi zinazoendelea, Dkt. Tulia amelipongeza Bunge la China kwa kuendelea kuwa Mwanachama makini na mwenye tija katika kuendeleza ajenda za IPU na kufikia malengo mbalimbali yanayokusudiwa Duniani ikiwemo kufikia malengo ya Maendeleo endelevu, harakati za kukomesha ugaidi, kuchagiza usawa wa kijinsia, maendeleo na ushirikishwaji Vijana na kuendeleza misingi na mashirikiano katika Umoja wa Mataifa Duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *